TULIFANYA KADRI YA UWEZO WETU

Licha ya kupoteza mchezo wa kwanza na wa pili wa mchujo wa fainali ya Ligi kuu ya kikapu nchini kwa wanaume nyumbani mjini Mombasa, kocha msaidizi wa mabingwa watetezi KPA Samuel Ocholla anaamini kwamba wachezaji walijitolea kwa kila hali na mali.
KPA ilipoteza mchezo wa kwanza alama 70-73 Jumamosi dhidi ya Nairobi City Thunder, kabla ya kupoteza wa pili kwa alama 50-59 Jumapili, msururu huo ukielekea Nairobi kwa michezo mitatu iliyosalia.
Thunder inasaka ushindi mmoja huku KPA ikilazimika kushinda michezo yote mitatu iliyosalia ili kutetea taji hilo.
Katika mchezo wa Jumapili ambao walipoteza kwa pointi tisa, Ocholla, nahodha wa zamani wa KPA, alisema walikosa uthabiti.
Imetayarishwa na Nelson Andati