TAASISI YA SILICON SAVANA YAZINDULIWA KUIMARISHA UHANDISI

Sekta ya uhandisi nchini imepigwa jeki baada ya Rais William Ruto kuzindua ujenzi wa taasisi ya kisasa ya uhandisi maarufu kama Silicon Savanah kuwezesha utafiti na uvumbuzi.
Ujenzi huo utaotekelezwa katika kipindi cha miaka 5 kwa gharama ya shilingi bilioni 3, utafanywa katika chuo kikuu cha Nairobi, ukifadhiliwa na serikali ya Ufaransa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais amesema ushirikiano huo utaokoa fedha nyingi, ikizingatiwa kuwa serikali yake hutumia asilimia 30 ya bajeti yake kwa sekta ya elimu kila mwaka.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa