#Business

SERIKALI: KRB KUFANYIWA MAREKEBISHO KUIMARISHA UBORA

Serikali kuu imependekeza kufanywa marekebisho mapya Bodi ya Barabara nchini KRB ili kuiwezesha kusimamia viwango vya jinsi barabara zitakavyorekebishwa na kujengwa na kutunzwa kwa viwango hitajika.

Kulingana Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen, sababu kuu za marekebisho ya bodi hiyo ni kuruhusu “kuzingatia ipasavyo miundo ya barabara na miongozo ya wanakandarasi na mashirika ya barabara.”

Aidha, waziri Murkomen amesema  serikali inatarajia Bodi na mashirika ya Barabara kuhakikisha kuwa kilomita 220,000 za barabara kuu za kitaifa zinakarabatiwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *