SABA ITATUZABA, WAKENYA WAPINGA MSWADA

Zoezi la kukusanya maoni ta wakenya kuhusu mswada wa kuongeza muhula wa Rais na viongozi wengine wanaochaguliwa kutoka miaka 5 hadi 7 linaendelea katika ukumbi wa mikutano KICC jijini Nairobi, leo ikiwa ndio siku ya mwisho.
Zoezi hilo linaongozwa na kamati ya haki na sheria katika bunge la kitaifa, lengo likiwa ni kupata mtazamo wa wakenya kuhusu mswada huo uliowasilishwa katika bunge la seneti na seneta wa Nandi Samson Cherargei.
Hata hivyo, wengi wa wakenya ambao wamezungumza wamepinga pendekezo hilo wakisema linaashiria kujitakia kwa viongozi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa