WANYONYI, MORAA WATIA FORA DIAMOND LEAGUE
Mshindi wa dhahabu ulimwenguni katika mbio za mita 800 za Olimipiki Emmanuel Wanyonyi ametia fora na kuibuka mshindi katika mashindano ya Diamnond League kwenye mbio hizo jana usiku nchini Uswizi, na kumpiku mshindani wake wa siku nyingi Marco Arop wa Canada.
Wanyonyi aliandikisha muda wa dakika 1. Sec 41.11, ukiwa ndio muda wa kasi zaidi tangu ule wa dakika 1.40.91 ulioadnikishwa na David Rudisha katika fainali za olimipiki za London mwaka 2012.
Bingwa wa dunia Arop, alilenga kumshinda Wanyonyi baada ya uhasama wa Olipimki zilizokamilika wiki chache zilizopita, ila akaambulia nafasi ya pili ingawa akapunguza mwanya wa muda
Katika mbio hizo kwa akina dada, bingwa wa dunia Mary Moraa aliweka nyuma masaibu yake ya Olimpiki za Paris ambako alimaliza wa tatu, ila jana akaibuka mshindi, na kuwapiku Georgia Bell wa Uingereza na Rekkie Jemma
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































