MAHAKAMA YAIDHINISHA KUONDOLEWA KWA SPIKA NYAMIRA
Aliyekuwa spika wa bunge la Nyamira Enock Okero aliondolewa afisini kisheria kulingana na uamuzi wa mahakama ambayo imetupilia mbali notisi zote zilikuwa zimetolewa na Okero.
Jaji wa mahakama kuu ya Bomet Julius Ng’aring’ari anasema vigezo vyote vya sheria vilizingatiwa wakati wa kubanduliwa kwake afisini.
Nafasi yake ilichukuliwa na mwakilishi wa wadi ya Ekerenyo Thaddeus Nyabaro.
Imetayarishwa na Maureen Makhobe
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































