#International

MVUA YAUA WATANO KUSINI MWA CHINA

Mvua kubwa imesababisha vifo vya watu watano na wengine kadhaa kupotea katika mikoa ya Guangdong na Guangxi nchini China.

Mamlaka zimetoa tahadhari za mafuriko ya milimani na majanga ya kijiolojia.

Kituo cha Kitaifa cha Hali ya Hewa kimetangaza tahadhari ya njano katika maeneo kadhaa kutokana na hatari ya mvua zaidi, huku mvua ikitarajiwa kuendelea hadi katika maeneo ya Xinjiang. Mwaka 2024 pia umetajwa kuwa na joto kali zaidi katika historia ya China.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *