MURKOMEN: MIZOZO YA ARDHI IMECHOCHEA UKOSEFU WA USALAMA
Kenya inakabiliwa na ongezeko la ukosefu wa usalama Kaskazini Mashariki kutokana na mizozo ya ardhi na mipaka, Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen amesema.
Akiwa Tharaka Nithi katika kongamano la Jukwaa la Usalama, Murkomen amesema mizozo hii imeenea katika kaunti nyingi na ni chanzo kikuu cha migogoro ya kijamii.
Aidha amehimiza utekelezaji wa ripoti ya Kikosi Kazi cha Okongo kuhusu utatuzi wa mizozo ya ardhi, na pia kugusia changamoto za migogoro kati ya binadamu na wanyamapori pamoja na kuongezeka kwa pombe haramu.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































