SERIKALI YAWATAKA WADAU KULINDA HADHI YA KCSE
Serikali imeendelea kuwataka walimu wakuu na wasimamizi wa mtihani wa kitaifa inayoendelea kuwa makini na kuzuia udanganyifu ili kulinda hadhi ya mtihani huo.
Akizungumza katika eneo la Kikuyu, katibu katika wizara ya elimu Belio Kipsang’ amewaonya wakurugenzi wa shule za kibinafsi dhidi ya kuwasaidia watahiniwa kushiriki udanganyifu akisema watachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha, ameahidi kupunguza idadi ya maafisa wa polisi wanaosimamia mtihani huo ili kuwaondolea hofu watahiniwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































