ULINGO WA SIASA WAPATA MGENI
Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua amezindua chama kipya cha Democracy for the Citizens Party DCP, anachopanga kukitumia kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2027.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Gachagua amesema anapanga kuzuru taifa zima akikusanya maoni ya wakenya kabla ya kuandika manifesto ya chama chake kipya.
Kinara wa chama hicho ni Gachagua mwenyewe, kaimu naibu wake akiwa seneta wa zamani wa Kakamega Cleophas Malala.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































