MWANAFUNZI WA MKU AMEPATIKA AKIWA AMEUAWA HUKO THIKA

Makachero wa idara ya upelelezi DCI wanachunguza kisa ambapo Faith Musembi mwanafunzi mwenye umri wa miaka 19 katika chuo kikuu cha MKU amepatikana ameuliwa katika mtaa wa pilot Thika kaunti ya Kiambu.
Inaarifiwa mwili wake uligunduliwa na babaye Bonface Musembi katika mtaa huo ulioko wadi ya hospital Thika.
Kwa mujibu wa babake marehemu alipokea simu jumatano wiki hii kutoka kwa mtu asiyemjua akishinikiza kupewa kikombozi cha shilingi elfu 20 ili kumwachilia bintiye.
Imebainika kwamba mtu huyo alitumia simu ya binti yake kuitisha kikombozi hicho.
Kulingana na Musembi mkewe alifanikiwa kuzituma fedha hizo ndiposa mwanawe aachiliwe ila hilo halikuzaa matunda.