#Local News

SITA WAKABILIWA NA KESI MAUAJI YA OJWANG

Washukiwa 6 akiwemo OCS wa kituo cha polisi cha Central jijini Nairobi Samson Taalam watarejeshwa mahakamani hii leo kufunguliwa rasmi kesi ya mauaji ya mwalimu na bloga Albert Ojwang aliyeuawa katika kituo hicho.

Hii ni baada ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma DPP Renson Ingonga kuidhinisha mashtaka ya mauaji dhidi yao, mamlaka ya kuchunguza mienendo ya polisi IPOA ikisema ina Ushahidi wa kutosha kuendesha kesi hiyo.

Washukiwa wengine ni maafisa wa polisi James Mukhwana na Peter Kimani, na wafungwa 3 waliokuwa kituoni humo usiku wa mauaji hayo.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *