#Local News

MWANAMUME MWENYE UMRI WA MIAKA 35 AUAWA KWA KUPIGWA RISASI ISIOLO

Maafisa wa idara ya upelelezi DCI wanachunguza mauaji ya mwanamume mwenye umri wa miaka 35 katika nyumba yake eneo la Aremet, Kaunti ya Isiolo.

Mwili wa Lonyiet Lodukai umepatikana ukiwa kwenye kichaka karibu na Shule ya Msingi ya Aremet katika eneo dogo la Aremet.

Maafisa wa polisi walitembelea eneo la tukio ambapo wamebaini kuwa marehemu alipigwa risasi upande wa kushoto wa kifua na risasi ikatoka upande wa kulia wa mgongo wake.

Polisi walisema bado hawajajua chanzo cha tukio hilo na kwamba mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi.

Imetayarishwa na Janice Marete

MWANAMUME MWENYE UMRI WA MIAKA 35 AUAWA KWA KUPIGWA RISASI ISIOLO

VIONGOZI WA MERU WAMTAKA MALALA KUJIEPUSHA NA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *