#Local News

WAZIRI WA KILIMO AWATAKA WAKULIMA KUKUMBATIA HUDUMA ZA NYANJANI ZA KILIMO KIDIJITALI

Huduma za nyanjani za kilimo ni muhimu sana katika kuhakikisha utoshelevu wa chakula,
Kulingana na waziri wa kilimo na ustawi wa mifugo Dkt. Andrew Karanja akiongeza kuwa maafisa wa kutoa huduma za nyanjani za kilimo huwapa wakulima ujuzi unaohitajika kwa lengo la kuhahikisha kilimo endelevu.

Dkt. Karanja, ameyasema haya wakati wa kuzindua kongamano kuhusu utoaji huduma za ushauri wa kilimo (KeFAAS).

Waziri huyo amesisitiza kuwa ufanisi wa mabadiliko katika sekta ya kilimo, utasababishwa na kuwepo kwa huduma za nyanjani za kilimo.

Aidha Karanja amedokeza kuwa sekta ya kilimo ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa taifa hili, kwa kuwa hubuni nafasi za ajira na kuchangia katika ukuaji wa maeneo ya mashinani.

Ili kufanyia mabadiliko sekta ya kilimo, Karanja amesema huduma za nyanjani ni sharti zikumbatiwe, hasaa katika viwango vya kaunti kwa kuwahusisha vijana walio na ujuzi wa kidijitali.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *