WAZAZI WAWATAKA WALIMU KURUDI SHULENI
Muungano wa kitaifa wa wazazi umewataka walimu kufutilia mbali mgomo wao ambao umeratibiwa kuanza wiki ijayo shule zitakapofunguliwa kwa muhula wa tatu.
Mwenyekiti wa kitaifa wa muungano huo Silas Obuhatsa, amehofia kudhoofika kwa masomo wakati huu ambapo wanafunzi wanafaa kujiandaa kwa mitihani ya kitaifa.
Aidha, ameitaka miungano ya walimu KNUT na KUPPET kuangazia upya uamuzi wao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































