#uncategorized

ELIJAH OBEBO AMEAPISHWA KAMA NAIBU GAVANA WA KAUNTI YA KISII

Elijah Obebo ameapishwa kuwa naibu gavana mpya wa kaunti ya Kisii Kiti cha Naibu Gavana wa Kisii kiliachwa wazi mapema mwaka huu kufuatia kutimuliwa kwa Robert Monda mwezi Februari kwa matumizi mabaya ya afisi, kukiuka katiba na utovu wa nidhamu uliokithiri.

Gavana Simba Arati mnamo Machi 2024, alimteua Elijah Obebo kwa kukaguliwa na kuidhinishwa na Bunge la Kaunti ya Kisii.Wawakilishi wadi 53 kati ya 70 wa kaunti ya kisii walipiga kura ya kuondolewa kwa Monda huku 15 wakipinga.

Baraza la Seneti la Kenya baadaye lilikubali kushtakiwa kwa Monda, na kuthibitisha uamuzi wa kumwondoa afisini.

Maseneta 39 walipiga kura kuunga mkono mashtaka manne yaliyowasilishwa dhidi ya Monda, huku Maseneta wanne wakipiga kura kupinga mashtaka hayo.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *