MSICHANA WA MIAKA 18 AJIUA KISUMU
Maafisa wa polisi eneo la Muhoroni kaunti ya kisumu wanachunguza kisa ambapo msichana mmoja amejitoa uhai kwa kujinyonga.
Mwili wa msichana huyo mwenye umri wa miaka 18 umepatikana na majirani ukininginia kwenye paa la nyumba yao , polisi wameuondoa mwili huo katika eneo la tukio na kuupeleka katika hifadhi ya maiti ukisubiri k,ufanyiwa upasuaji ili kubaini chanzo cha kifo chake.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































