AMBROSE RACHIER AREJEA KUONGOZA GOR MAHIA

Ambrose Rachier amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa klabu ya Gor Mahia baada ya uchaguzi mkali uliofanyika katika uwanja wa Nyayo
Wakili huyo wa jijini alipata kura 658 dhidi ya mpinzani wake pekee, aliyekuwa mweka hazina wa klabu hiyo, Dolfina Achieng’, aliyepata kura 456.
Rachier alichukua uongozi wa K’Ogalo mwaka 2008 na tangu wakati huo ameiongoza klabu hiyo kupata mafanikio makubwa, ikiwemo kutwaa mataji tisa ya Ligi Kuu ya FKF na kombe moja la ndani.
Uchaguzi wa Jumapili unamaanisha kwamba Rachier anaweza kuongoza hadi mwaka 2029, na hivyo kufikisha miaka 21 madarakani.
Imetayarishwa na Janice Marete