RUTO AFICHUA ‘MFADHILI’ WA VURUGU
Rais William Ruto amelitaja shirika lisilo la kiserikali la Marekani kama wafadhili wa vurugu zilizoshuhudiwa humu nchini wakati wa maandamano ya kupinga mzigo wa ushuru.
Akizungumza katika kaunti ya Nakuru, na kisha kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X, Ruto amesisitiza kwamba shirika hilo liliwalipa wahuni kuharibu mali na kupora biashara.
Aidha, Ruto amesema serikali yake haitasita kuwakabili kisheria wanaowatumia vijana visivyo.
Aidha, Ruto ametishia kuiondoa Kenya katika mahakama ya haki ya Afrika Mashariki EACJ iwapo mahakama hiyo haitaondoa marufuku iliyowekwa kuhusu umiliki wa misitu nchini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































