POLISI WAATHIRWA WAKUBWA, KANJA AFICHUA

Katika juhudi za kuboresha utendakazi wa polisi na kuimarisha huduma yao kwa wananchi, Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja ameongoza mkutano wa kujadili matatizo ya akili na msongo wa mawazo miongoni mwa maafisa hao ili kupata suluhu.
Kongamano hilo ambalo limeandaliwa jijini Nairobi limewaleta Pamoja maafisa wakuu wa idara ya polisi na wale wa upelelezi ambako polisi wamehimizwa kutafuta usaidizi wanapokabiliwa na matatizo ya msongo wa mawazo.
Kwa mujibu wa Kanja, polisi ndio waathirwa wakubwa wa matatizo hayo ikilinganishwa na raia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa