MWAURA: SERIKALI KUKAGUA MIRADI KOTE NCHINI
Serikali imetengaza kuendesha zoezi la kukagua miradi yote nchini iliyoanziasha, msemaji wa serikali Isaac Mwaura akifichua haya baada ya kuibuka ripoti kwamba kuna miradi ambayo imtelekezwa huku nyingine ikikabiliwa na Sakata za ufisadi.
Katika kikao na wanahabari jijini Nairobi, Mwaura amesema kwamba maafisa kutoka afisi ya rais watafanya ukaguzi wa kina katika maeneo yote ya taifa kwa lengo la kubaini hali halisi ya miradi ya maendeleo.
Aidha, amesisitiza kwamba lengo la zoezi hilo ni kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa mujibu wa malengo ya uzinduzi wake, na kuongeza kwamba serikali inajitahidi kuboresha masoko.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































