#Football #Sports

KODEROBARA WATUA UBINGWA NYANZA

Shule ya upili ya Koderobara ndio mabingwa wapya wa ukanda wa Nyanza kwenye mashindano baina ya shule za uili muhla wa pili.

Koderobara, inayowakilisha kaunti ya Migori, iliibuka washindi baada ya kuwaondoa Matutu PAG kutoka Nyamira kwa mabao 2-1, katika mechi ya fainali iliyochezwa katika uwanja wa Moi mjini Kisumu.

Mechi hiyo iliahirishwa kutoka Jumamosi wiki jana baada ya umati kuzua fujo wakati wa mechi ya nusu fainali kati ya Agoro Sare na Matutu katika uwanja wa Kadinali Otunga, Mosocho, ambayo baadaye ilitiuka wakiongoza kwa mabao 2-0.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, kocha wa Koderobara Moses Otieno alitoa onyo kwa wapinzani wao kwamba wanakuja kali kwenye ubingwa wa kitaifa.

Mabingwa hao wa Kaunti ya Migori sasa watawakilisha Kanda ya Nyanza katika fainali zinazotarajiwa kuanza tarehe 29 mwezi huu, hii ni kwa vile kesi iliyowasilishwa na Agoro Sare kwenye mechi yao iliyotibuka dhidi ya Matutu bado haijakamilika.

Imetayarishwa na Nelson Andati

KODEROBARA WATUA UBINGWA NYANZA

SIJUI LOLOTE ASEMA POSTECOGLOU

KODEROBARA WATUA UBINGWA NYANZA

AUSTRALIA YAMNYAKUA MATHEW RYAN

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *