SHABANA YAILAZA KENYA POLICE FC BAO 1-0

Shabana waliifunga Kenya Police FC 1-0 Jumapili jioni na kupata ushindi wao wa kwanza wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Soka ya Kenya (FKF) kwenye Uwanja wa Gusii, Kisii. Vincent Nyabuto alifunga bao pekee katika dakika ya 35, akiruka juu kukutana na krosi ya James Mazembe kutoka upande wa kushoto, huku kipa wa Police Patrick Matasi akiangalia bila msaada.
Walinda usalama, wakiwa na nia ya kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza, wangeweza kupata uongozi katika dakika ya tisa lakini shuti la chini la Francis Kahata — kufuatia pasi ya David Okoth — liligonga upande wa nje wa mlingoti.
Alfred Mang’eni kisha akapiga kichwa nje katika dakika ya 20 kutoka kona ya kuelea kabla ya Matasi karibu kuwapa Tore Bobe bao la kwanza katika dakika ya 24. Kipa huyo wa Harambee Stars alilazimika kumshukuru nyota yake ya bahati au tuseme beki wa kulia Daniel Sakari — baada ya kukosa kabisa kuudaka mpira wa krosi kutoka upande wa kulia.
Mpira ulianguka miguuni mwa Kevin Omondi ambaye kusita kwake ndani ya boksi kulimruhusu Sakari kuondosha mpira kabla hajapiga shuti.
Afande walijibu kwa nafasi yao wenyewe, ambapo shuti la mguu wa kushoto la Okoth kutoka nje ya boksi karibu likampita Stephen Ochieng aliyekuwa langoni kwa Shabana.
Kutoka kwenye juhudi zilizokuwa zikipoteza matumaini, Shabana walipata bao walilolihitaji sana.
Imetayarishwa na Janice Marete