BAYERN WAMNYAKUA OLISE

Bayern Munich wamemsajili mshambuliaji wa Ufaransa Michael Olise kutoka Crystal Palace,
Bayern ililipa kifungu cha kutolewa cha euro milioni 70 ($75 milioni) kwa klabu hiyo ya Ligi Kuu ili kupata huduma ya Olise kwa mkataba wa miaka mitano.
Olise, 22, alikamilisha matibabu katika mji mkuu wa Bavaria siku ya Jumapili.
Olise mzaliwa wa London, amewakilisha timu za vijana za Ufaransa na atachezea Les Bleus chini ya kocha Thierry Henry kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris mnamo Agosti.
Olise alifunga mabao 10 katika michezo za Ligi Kuu msimu uliopita kwa klabu hiyo ya London.
Yeye ni ujio wa pili kuu wa Bayern katika msimu huu baada ya beki wa Japan Hiroki Ito aliyewasili kutoka Stuttgart.
Bayern ilimaliza ya tatu nyuma ya mabingwa Bayer Leverkusen na Stuttgart msimu uliopita, na kuvunja msururu wa mataji 11 mfululizo ya Bundesliga.
Mbali na nahodha wa Uingereza Harry Kane, ambaye alifunga mabao 36 katika michezo 32 ya Bundesliga, Bayern walitatizika kutafuta mabao msimu uliopita, huku Jamal Musiala pekee (mabao 10) akifikisha idadi mbili.
Imetayarishwa na Nelson Andati