MASENGELI AJIPATANISHA NA MAHAKAMA, AAHIDI USHIRIKIANO

Hatimaye naibu inspekta mkuu wa polisi katika kitengo cha polisi wa utawala Gilbert Masengeli, ameomba msamaha kwa mahakama iliyompata na hatia ya kupuuza mahakama alipodinda kufika mahakamani kutoa maelezo kuhusu walikokuwa wakenya 3.
Masengeli ambaye amekuwa akihudumu kama kaimu inspekta mkuu wa polisi, alihukumiwa kifungo cha miezi 6 gerezani ila kifungo hicho kikafutiliwa mbali kwa siku 7 ili kumwezesha ajiwasilishe mahakamani.
Licha ya kutaja majukumu ya kikazi kuwa sababu za kukosa kufika mahakamani, Masengeli ameahidi kutii sheria na kushirikiana na mahakama siku zijazo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa