#Local News

MWANAUME WA EMBAKASI ANASAKWA NA POLISI BAADA YA KUDAIWA KUMUUA MKEWE

Polisi wanamsaka mshukiwa wa mauaji ya mkewe katika mtaa wa mabanda wa Mukuru, Nairobi.

Mwili wa Maria Anami umepatikana kwenye dimbwi la maji ukiwa umewekwa jiwe juu yake.

Hii ilikuwa baada ya kupigwa kichwani na kufariki muda mfupi baadaye katika ugomvi na mumewe.

Kulingana na polisi, mume alikuwa amempigia simu jamaa yake kumwarifu mkewe alikuwa amefariki.

Hii ilikuwa baada ya kudaiwa kuhusika naye katika ugomvi kuhusu madai ya usherati.

Mshukiwa huyo alimweleza jamaa kuwa alikuwa amempata mwanamke huyo na mwanamume mwingine na kusababisha ugomvi ambao uligeuka kuwa kifo

Imetayrishwa na Janice Marete

MWANAUME WA EMBAKASI ANASAKWA NA POLISI BAADA YA KUDAIWA KUMUUA MKEWE

KIFUNGO CHA MIAKA 20 JELA KWA MWANAMKE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *