GAVANA WA KIRINYAGA ANN WAIGURU ALALAMIKIA MAUAJI YA WANAWAKE NCHINI

Gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru amelalalamikia ongezeko la mauaji ya wanawake nchini na kutoa wito kwa polisi kusitisha mauaji hayo mara moja.
Waiguru aidha ametoa wito kwa taasisi za upelelezi kuharakisha uchunguzi juu ya kiini cha mauaji hayo ili wahusika wakabiliwe kwa mujibu wa sheria kwa kuwa Kulingana naye hatua hiyo itasaidia kukomesha mauaji hayo nchini.
Ameongeza kuwa mauaji hayo ya yanayoripotiwa mara kwa mara ni ya kutatanisha ni ya kushangaza na kwamba hatua za tharura zinapaswa kuchukuliwa.
Imetayarishwa na Janice Marete