WAADHIRIWA WA MKASA WA MAIMAHIU WAONDOLEWA KAMBINI

Serikali imeanza mchakato wa kuvunja kambi zilizokuwa zikihifadhi waadhiriwa wa mafuriko ya Mai Mahiu yaliyotokea Aprili 29, 2024.
Hatua hiyo inalenga kuwezesha waathiriwa kurejelea maisha yao baada ya mkasa huo uliogharimu maisha ya zaidi ya watu 6o, kusomba nyumba na kuwaacha wengine na majeraha.
Wiki jana, kamati ya usimamizi wa majanga iliambatana na waathiriwa waliokuwa wamehifadhiwa katika Makao ya Watoto ya PBB hadi ardhi yao iliyoharibiwa, kwa nia ya kuwatambua wamiliki halali wa sehemu za ardhi ambapo nyumba zilisombwa na mafuriko.
Imetayarishwa na: Janice Marete
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































