#Local News

GAVANA MUTHOMI NJUKI APENDEKEZA KAUNTI KUPEWA JUKUMU LA KUNUNUA NA KUSAMBAZA MBOLEA KWA WAKULIMA

Gavana wa kaunti ya Tharakanithi Muhomi Njuki ameitaka serikali ya kitaifa kuzipa serikali za kaunti jukumu la kununua na kusambaza mbolea kwa wakulima.

Akizungumza mjini Mombasa katika kongamano la kilimo Muthomi amesema kiuwa mbolea ambayo imekuwa ikisambazwa kwa wakulima imeripotiwa kuwa tofauti na ile inayohitajika, akiongeza kuwa kuna baathi ya wakulima ambao wam ekuwa wakipewa mbolea ya mahindi wakati ambapo wanajihusisha na kilimo tofauti.

Muthomi aidha ameitaka serikali ya kitaifa kutengea serikali za kaunti pesa za kununua mbolea stahiki ili wakulima wasambaziwe bila matatizo yoyote.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *