#Local News

‘KATIBU MKUU BANDIA’ UDA AJERUHIWA

Joe Khalende aliyejitangaza kuwa katibu mkuu wa chama tawala cha UDA sasa anauguza majeraha baada ya kusambuliwa na watu wanachama wanaoaminika kuwa wafuasi wa katibu mkuu Cleophas Malala katika makao makuu ya chama hicho.

Khelende amepata majeraha kichwani, akidai kwamba kuna watu walio na njama ya kummwangamiza.

Kundi la watu waliomshambulia limekuwa likiimba nyimbo za kumsifia Malala.

Awali, mwenyekiti wa UDA Cecil Mbarire, alipinga madai ya kwamba Khalende ndiye katibu mkuu mpya wa chama hicho.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *