#Local News

“TUOKOLEE NZOIA YETU” GAVANA LUSAKA

Katika juhudi za kuhakikisha wakulima wa miwa katika kiwanda cha sukari cha Nzoia wanaboresha Maisha yao, gavana wa Bungoma Ken Lusaka amemwomba Rais William Ruto kuingilia kati na kutatua matatizo ya kifedha kwenye kiwanda hicho.

Akizungumza katika eneo la Mumias kaunti ya Kakamega ambako Rais amezindua bonasi kwa wakulima wa miwa, Lusaka amekariri haja ya kufufua kiwanda hicho ambacho kinatgemewa na wengi wa wakazi wa Bungoma.

Rais ambaye anafanya ziara ya wiki moja eneo la Magharibi, ameratibiwa kuzuru kaunti ya Bungoma Alhamisi wiki hii.

Hata hivyo, Rais Ruto ameahidi mageuzi katika sekta ya miwa ili kuwanufaisha wakulima.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *