WIZARA YA AFYA YATHIBITISHA KISA CHA TANO CHA MPOX NCHINI KENYA
Kenya imethibitisha kisa chake cha tano cha Mpox kinachomhusisha mwanamke mwenye umri wa miaka 29 anayeishi karibu na Chuo cha Tumaini huko Mombasa.
Katika taarifa, Waziri wa Afya Deborah Barasa ameeleza kuwa mwanamke huyo alipata virusi hivyo kutoka kwa mwenziwe, ambaye alikuwa kisa cha nne kuthibitishwa nchini na kwa sasa amelazwa hosipitali.
Mwanamke huyo amelazwa katika Hospitali Kuu ya Pwani baada ya vipimo kubadilika, alitengwa katika Kituo cha Kutengwa cha Hospitali ya Utange cha Mpox.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































