SILIBWET INA MATUMAINI KUFANYA VYEMA

Meneja wa Timu ya Silibwet Leons inayokabiliwa na hatari ya kushuka daraja, Eric Rono, bado ana matumaini kwamba watabadili msimu mbaya na kunusurika.
Baada ya kucheza kwa raundi 34, Leons wapo mkiani mwa msimamo wa ligi wakiwa na pointi 22, na wanaweza kushushwa Daraja hadi daraja la tatu iwapo watashindwa kusajili ushindi katika mechi zao nne zilizosalia.
Rono ametaja uhaba wa fedha kuwa sababu kuu inayochangia kutofanya vizuri kwao msimu huu.
Meneja wa timu hiyo hata hivyo amekerwa na hatua ya FKF ya kuwapokonya pointi kwa kukosa kufika uwanjani kwa pambano lao dhidi ya Mombasa Stars, akidai kuwa si haki na anataka uamuzi huo uangaliwe upya.
Timu hiyo itamenyana na vinara Mara Sugar katika mchezo wao ujao wa ligi siku ya Jumamosi.
Imetayarishwa na Nelson Andati