#uncategorized

SERIKALI IMEWEKA MIKAKATI YA KUFANIKISHA MASOMO KATIKA SHULE ZA MSINGI

Serikali imeweka mikakati yote kufanikisha masomo ya wanafunzi wa shule ya msingi kinyume na usemi wa baadhi ya wakenya haya yakiwa ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa masomo ya shule za msingi katika wizara ya elimu Dkt Stephen Balongo ambaye alimwakilisha katibu Belio Kipsang katika hafla ya kuadhimisha siku ya elimu eneo la samia kaunti ya Busia.


Kwa mujibu wa barongo miundo msingi katika shule pia itaboreshwa ili kuimarisha usalama na mazingira mbadala ya wanafunzi kuendeleza masomo yao.


Kwa upande wake gavana wa busia dkt Paul Otwomo aliyekuwa katika hafla hiyo amesema licha ya serikali kuonyesha nia ya kuboresha masomo hatua ya kuondoa pesa za lishe shuleni kwenye bajeti ya 2024-2025 haifai kamwe kwa kuwa lishe hiyo imekuwa afueni kwa wanafunzi kwa muda mrefuOtwomo vile vile ameongeza kuwa serikali za kaunti hazipaswi kunyimwa ruhusa kupeana basari kwa wanafunzi kutoka familia maskini.

Imetayarishwa na: Janice Marete

RATIBA YA RAIS RUTO ANAPOANZA ZIARA YA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *