BOSI MPYA WA FKF KORIR ANA IMANI KUWA ATAHUDUMU KWA MAFANIKIO LICHA YA HOMA YA UCHAGUZI
Afisa Mkuu Mtendaji wa Muda wa Shirikisho la Soka la Kenya Patrick Korir ana imani ataliongoza shirikisho hilo vyema licha ya uteuzi wake ambao unajiri wakati uwanja wa soka wa humu nchini ukiwa na homa ya uchaguzi.
Uteuzi wa Korir kwa muda ulithibitishwa siku ya Jumanne kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji Barry Otieno, ambaye alihudumu katika wadhifa huo tangu 2019 alipochukua uongozi kutoka kwa Robert Muthomi.
Korir anasema lengo lake la haraka litakuwa kuhakikisha uendeshaji mzuri wa shughuli za kila siku za shirikisho hilo, zaidi katika muktadha wa maandalizi ya uchaguzi wa Desemba 7.
Afisa Mkuu Mtendaji Mkuu wa Nairobi City Stars anasema itakuwa fursa nzuri kutumikia nchi katika wadhifa huo licha ya sintofahamu inayotokana na uteuzi wake wa muda.
Imetayarishwa na Janice Marete.
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































