EVANS ASHINDA SAFARI RALLY KENYA, AIMARISHA UONGOZI WRC
Elfyn Evans ameongoza Mashindano ya Dunia ya WRC baada ya kushinda Safari Rally Kenya. Dereva wa Toyota sasa anaongoza kwa alama 36 mbele ya Thierry Neuville baada ya raundi tatu.
Evans aliepuka changamoto za Safari Rally na kumaliza na uongozi wa dakika 1 na sekunde 9 mbele ya Ott Tanak wa Hyundai. Neuville alimaliza wa tatu, huku Takamoto Katsuta akinusurika ajali na kusaidiwa na mashabiki.
Mashindano ya WRC yataendelea Aprili kwenye Canary Islands.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































