MASENGELI AADHIBIWE KWA KUKAIDI AMRI ZA MAHAKAMA – WAKILI KHAMINWA
Hakuna aliye juu ya sheria, haya ni kwa mujibu wa Wakili John Khaminwa akimtaka Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli aadhibiwe kwa kutotii maagizo ya mahakama.
Kulingana na Khaminwa hakuna aliye juu ya sheria kukataa kimakusudi kuheshimu amri za mahakama.
Wakili huyo Mwandamizi amesisitiza kuwa amri za mahakama lazima zizingatiwe na wote na kuongeza kuwa yeyote atakaekaidi lazima akabiliwe na hukumu na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
Imetayrishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































