#Football #Sports

HIGHWAY YAPITA NA KITALE

Mabingwa wa Nairobi Highway walizamisha St. Joseph’s Kitale 1-0 na kuanza harakati zao za kuwania taji la taifa la kandanda kwa njia ya kutatanisha, Michezo ya Shule ya Sekondari ya Kidato cha Pili ilipong’oa nanga mjini Kisii Jumapili.

Katika Uwanja wa Gusii uliojaa, timu hiyo inayonolewa na Beldine Odemba ilionyesha utulivu dhidi ya mabingwa hao wa Bonde la Ufa, na kupata ushindi huo muhimu ambao kocha huyo anasema ulistahili.

Mechi ya ufunguzi kati ya Kodero Bara ya Nyanza na Kirangari High kutoka Central ilimalizika kwa sare ya 2-2. Kocha mkuu wa Kodero Bara Moses Otieno anatumai watashinda katika mechi yao ya pili dhidi ya Musingu High.

Katika uwanja wa Cardinal Otunga High Mosocho, Musingu High uliilaza Shule ya Machakos 1-0. Katika soka ya wasichana, Dagoretti Mixed ya Nairobi iliichapa Alara girls bao 1-0 kwenye uwanja wa Gusii, huku mechi ya Kombani na St. Joseph ikimalizika kwa sare ya 1-1.

Nyakach Girls iliidhalilisha Kinale kwa mabao 3-1 huku Butere Girls ikiilaza Kibauni 1-0. Mashindano yanaingia siku ya II Jumatatu.

Imetayarishwa na Nelson Andati

HIGHWAY YAPITA NA KITALE

TUTAJARIBU TENA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *