PASSARIS AAPA KUUNGA MKONO MSWADA WA KIFEDHA

Mwakilishi wa kike katika kaunti ya Nairobi Esther Passaris amesema ataunga mkono mswada tata wa fedha wa mwaka 2024-25, na kwamba hatatishwa na mtu yeyote.
Katika video inayosambaa mtandaoni, Passaris vile vile amepuzilia mbali shinikizo ya mrengo wa Azimio kuwataka wabunge wake kuupinga mswada huo.
Amesema ni jukumu la kila Mkenya kulipa ushuru kwa maendeleo ya taifa.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa