#Sports

HATUA ZA KIDHARURA ZICHUKULIWE

Waziri la Michezo Kipchumba Murkomen anataka hatua za haraka zichukuliwe ili kupanua uwakilishi wa Kenya katika Michezo ya Olimpiki kwa siku za usoni, akisisitiza haja ya kuzingatia michezo yenye kukosa uwakilishi kutoka Kenya na kuimarisha maandalizi ya mapema.

Akizungumza katika warsha ya kimkakati ya Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki ya Kenya (NOC-K) mjini Sagana, Murkomen aliwataka wadau wa michezo kuongeza juhudi zao katika kuhakikisha mustakabali wa Olimpiki wa Kenya unajumuishwa zaidi katika taaluma mbalimbali.

Warsha hiyo, iliyopitia matokeo ya Kenya katika Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 na kupanga mikakati ya Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Dakar 2026 na Olimpiki ya Majira ya joto jijini Los Angeles 2028, ilileta pamoja viongozi wa mashirikisho tofauti ya michezo nchini na wataalam wa kiufundi.

Waziri huyo aliangazia umuhimu wa mkutano huo, akiashiria kuwa ni mara ya kwanza katika historia ya Kenya kwa kikao cha mkakati kama hicho kufanywa ndani ya miezi miwili baada ya kukamilika kwa Michezo ya Olimpiki.

Alisisitiza umuhimu wa maandalizi ya mapema na ushirikiano wa karibu kati ya mashirikisho, wachezaji, na timu za kiufundi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

HATUA ZA KIDHARURA ZICHUKULIWE

HUSSEIN ATAKA UCHAGUZI WA HURU NA HAKI

HATUA ZA KIDHARURA ZICHUKULIWE

MATAIFA YA AFRIKA MASHARIKI WASHIRIKI MCHUJO WA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *