TEKELEZENI AFCFTA, AFRIKA YASHAURIWA

Nchi za Afrika zimetakiwa kutoa mipango kazi na mikakati ya kitaifa ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) na maingiliano ya kiuchumi baina ya nchi hizo.
Wito huo umetolewa katika Jukwaa la Majadiliano ya Kitaifa kuhusu Maendeleo ya Mkakati wa Utekelezaji wa eneo la biashara huria nchini Ethiopia lililofanyika mjini Addis Ababa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Idara ya Maingiliano ya Kikanda na Biashara iliyo chini ya Tume ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa, Stephen Karingi, amesema utekelezaji wa vitendo vya eneo la biashara huria una fursa nzuri ya kuendeleza mageuzi ya viwanda, utoaji wa nafasi za ajira, na uwekezaji barani Afrika.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi