KARUA: MNAWATUMIA WANAJESHI VIBAYA
Muda mfupi baada ya bunge kuidhinisha kutumkwa kwa wanjeshi kwenye operesheni ya kurejesha utulivu nchini, kinara wa chama cha Narc Kenya Martha Karua ameshutumu hatua hiyo, akisema serikali inawatumia wanajeshi kulinda maslahi ya baadhi ya viongozi.
Katika taarifa kwa wanahabari, Karua aidha ameshutumu visa vya maafisa wa polisi kutumia nguvu kupita kiasi kuwakabili waandamaji.
Aidha, Karua amewataka maafisa wa vikosi vya usalama kutotumiwa vibaya, akisema watawajibishwa binafsi kisheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































