WADAU WAOMBA WALIMU PWANI
Washikadau wa elimu katika ukanda wa pwani wametaja uhaba wa walimu na wanafunzi kukosa kuhudhiria vipindi vya masomo katika shule za umma kama changamoto kuu zinazoathiri elim.
Wakizungumza kwenye kongamano la elimu katika shule ya Bomu eneo la Changamwe, washikadau hao wametoa wito kwa serikali kuwaajiri wlaimu zaidi, wakidai kwamba asilimia 50 ya walimu ukanda huo wameajiriwa na bodi za shule.
Aidha, wametoa wito kwa wazazi kuhakikisha kwamba Watoto wao wanafika shuleni kwa masomo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































