#Business

KENGEN KUSAKA NJIA MBADALA YA UZALISHAJI

Shirika la kuzalisha umeme KenGen limesema inapanga kupunguza utegemezi wa umeme wa maji nchini ili kuimarisha ustahimilivu wa nishati, likisema umeme wa aina hiyo unaweza kuathiriwa na mvua isiyotabiriwa.

Afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo Peter Njenga amesema uwezo wa umeme wa maji nchini Kenya unakadiriwa kuwa megawati 840, ambao unachukua asilimia 24 ya uzalishaji wa jumla wa umeme.

Kwenye taarifa jijini Nairobi, Njenga amesema umeme wa maji ni chanzo imara cha nishati chenye bei nafuu zaidi, lakini pia kinaweza kuathiriwa kirahisi zaidi na mabadiliko ya tabia nchi. Ameongeza kuwa kwa vile sasa ukame unaathiri vibaya uzalishaji, utegemezi wa mabwawa ya maji nchini humo unatathminiwa upya

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

KENGEN KUSAKA NJIA MBADALA YA UZALISHAJI

MAHAKAMA YASITISHAI MCHAKATO WA IEBC

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *