#Local News

MAHAKAMA YAIDHINISHA KUAPISHWA KWA USIMAMIZI WA IEBC

Mwenyekiti mpya wa IEBC Erastus Ethekon na makamishna 6 wanatarajiwa kuapishwa muda wowote baada ya mahakama kuu kutupilia kesi iliyokuwa ikipinga mchakato uliotumika kuwapiga msasa na kuwateua.

Kwenye uamuzi wake, jopo la majaji 3 Roselyn Aburili, John Chigiti na Bahati Mwamuye wamesema kesi hiyo iliyowasilishwa na Kelvin Omondi na Boniface Mwangi haikuzingatia vigezo hitajika chini ya kipengee cha 22 cha katiba.

Makamishna wanaotarajiwa kuapishwa na mwenyekiti huyo ni Ann Nderitu, Alutalala Mukhwana, Mary Sorobit, Hassan Noor Hassan, Francis Odhiambo, na Fahima Araphat Abdallah.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MAHAKAMA YAIDHINISHA KUAPISHWA KWA USIMAMIZI WA IEBC

TUKO TAYARI KWA CHAN

MAHAKAMA YAIDHINISHA KUAPISHWA KWA USIMAMIZI WA IEBC

KAULI YA MBUNGE YASHTUA NCHI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *