SOFAPAKA ANA MATUMAINI MAKUBW AKWA KIKOSI CHAKE
Kocha mkuu wa Sofapaka Robert ‘The Lion’ Matano anatumai timu yake itaendeleza kasi ya ushindi baada ya kupachika ushindi wao wa kwanza msimu huu, ushindi mgumu wa 1-0 dhidi ya Shabana FC katika FKF-PL.
Mtaalamu huyo wa zamani wa Tusker na AFC Leopards anaamini ‘Batoto Ba Mungu’ itakusanya pointi nyingi zaidi kutoka kwa mechi 28 zilizosalia ili kumaliza katika nafasi ya heshima licha ya kuanza polepole kwa kampeni ya sasa.
Katika mechi hizo 28, tutaendelea kufanya mazoezi kwa bidii na kujaribu kushinda mechi moja kwa wakati mmoja.
Nadhani baada ya mechi 28, Sofapaka itakuwa mahali fulani,” Matano alisema.
Matano, hata hivyo, amewaonya wachezaji wake dhidi ya kuridhika na msisimko kupita kiasi na anataka wapiganie kila kitu.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































