#Local News

“SITAKI KUITWA ZAKAYO PEKEE YANGU” RUTO

Rais William Ruto amesema kwamba lengo lake la kubuni serikali pana kwa ushirikiano na mrengo wa upinzani ni kuliunganisha taifa ili kuafikia mageuzi ya kiuchumi.

Akizungumza katika eneo la Rukuriri kaunti ya Embu, Rais amesema hatua hiyo itadhibiti kauli za uchochezi na kutoa fursa kwa taifa kuangazia ajenda yake ya maendeleo.

Aidha, amesema kupitia serikali pana, taifa linaweza kukusanya ushuru kwa Pamoja bila yeye kubebeshwa lawama binafsi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *