#Local News

AFISA WA KAUNTI YA MIGORI ACHUNGUZWA KWA KUMSHAMBULIA DEREVA WA LORI KWA KUKOJOA HADHARANI

Polisi kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Migori wanamchunguza afisa wa polisi wa kaunti ambaye anadaiwa kumpiga dereva wa tipper kwa madai ya kukojoa eneo la wazi ndani ya mji wa Rongo, Kaunti Ndogo ya Rongo.

Shambulio hilo limewafanya wahudumu wa lori katika mji wa Rongo kuangusha zana zao na kupinga mienendo ya maafisa wa kutekeleza sheria katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa SACCO ya Rongo Pius Onyango amesema kuwa dereva dereva huyo amepata majeraha mabaya kichwani.

Oyango ambaye aliongoza wasafirishaji hao katika maandamano anaitaka serikali ya kaunti ya Migori kuhakikisha kuwa afisa wa utekelezaji anakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Mjumbe wa kamati kuu ya kaunti ya Migori anayesimamia usimamizi wa utumishi wa umma John Kobado amesema suala hilo linachunguzwa na watachukua hatua za kisheria baada ya uchunguzi kukamilika.

Kobado aidha ameongeza kuwa vitendo kama hivyo havifai na kuwaonya wafanyikazi wa serikali ya kaunti dhidi ya kuwadhulumu wakaazi.

Imetayarishwa na Janice Marete

AFISA WA KAUNTI YA MIGORI ACHUNGUZWA KWA KUMSHAMBULIA DEREVA WA LORI KWA KUKOJOA HADHARANI

HATMA YA JOPO LA MAJAJI 3 KUBAINIKA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *