VIONGOZI WA MERU WAMTAKA MALALA KUJIEPUSHA NA MASWALA YA KAUNTI YA MERU
Baadhi ya viongozi wa kaunti ya Meru wamemsuta katibu mkuu wa chama cha UDA Cleophus Malala kwa kumlaumi naibu kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya Meru Ziporah Kinya kwa hatua yake ya kuwasilisha bungeni mswada wa kumbandua mamlakani gavana wa kaunti hiyo kawira mwangaza.
Wakiongozwa na seneta wa kaunti hiyo Kathuri Murungi viongozi hao wamemtaka Malala kujiepusha na siasa za kaunti ya Meru.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































