MCAS 2 WA MAKUENI KUFIKA MBELE YA DCI ALHAMISI

Idara ya usalama imezidisha msako dhidi ya wanasiasa wanaoaminika kufadhili vurugu na uharibifu wa mali ulioshuhudiwa wakati wa maandamano ya vijana wiki jana, wawakilishi wadi wawili katika kaunti ya Makueni wakiwa miongoni mwa watu wanaochunguzwa.
Wawili hao ambao ni Albanus Wambua na Francis Mutuku wameagizwa kufika katika makao makuu ya DCI hii leo, baada yao kujiwasilisha katika afisi za DCI katika kaunti hiyo hapo jana.
Polisi wanaamini wawili hao ndio wahusika wakuu katika vurugu zilizoshuhudiwa kwenye kaunti hiyo licha yao kukana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa